Posted in

Hatari 10 Zinazoweza Kuiangusha Biashara Yako

Katika kila uwekezaji, jambo la hakika zaidi siyo faida  ni hatari. Faida ni kitu tunachokitamani, lakini hatari ni kitu
ambacho lazima tukabiliane nacho. Na kama hujui hatari zako ni zipi, basi tayari umejiandaa kushindwa, hata kama
hujui.

Swali hili Unaelewa Vema Hatari Zinazoweza Kuiangusha Biashara Yangu”  linagusa moyo wa uwekezaji wowote.
Si kila mradi unaanguka kwa sababu watu walikuwa wavivu au walikosa mtaji mara nyingi unaanguka kwa sababu Unaiingia bila ramani ya hatari. Uliamini mambo yataenda sawa, ukasahau kuwa mazingira ya biashara hubadilika kwa kasi, watu hubadilika, soko hubadilika, na mifumo pia hubadilika.Wengi wamewekeza mamilioni, wakajikuta baada ya miaka
miwili: Bidhaa zao hazihitajiki tena.
Bei imeshuka ghafla ,wameingia sokoni ambako kuna wadau wachache ndio
wanaotawala.Au wameshindwa kulipa mishahara kwa sababu hawakujua gharama zitapanda.Hatari hizi haziji na king’ora  zinakuja taratibu, na kabla hujajua, mradi mzima umeporomoka

1. Kushuka kwa bei ghafla
Mazao kuzidi mahitaji (oversupply) Mabadiliko ya hali ya hewa yanayoathiri mavuno Kuongezeka kwa mazao mbadala sokoni Kushuka kwa bei ya kimataifa
2. Hatari za Washindani Washindani wapya kuingia na bei nafuu  Washindani wenye teknolojia bora au mbinu mpya
Washindani kutoa huduma bora zaidi kwa wateja Kushindwa kuendelea na kasi ya ushindani wa soko.
3.Hatari za Fedha kukosekana kwa mpango wa mzunguko wa fedha (cash
flow) kutegemea chanzo kimoja cha mapato madeni mengi yasiyolipika kwa wakati kukosekana kwa akiba ya dharura
Kutokuwa na usimamizi mzuri wa matumizi
4.Hatari za Soko mabadiliko ya mahitaji ya wateja kupungua kwa uaminifu wa wateja
Kuingia kwa bidhaa mpya zinazobadilisha soko kutotangaza au kutafuta masoko mapya
5. Hatari za Sheria na Sera za Serikali Sheria mpya au mabadiliko ya kanuni za biashara kodi mpya au ongezeko la tozo
Vikwazo vya kibiashara au leseni kugoma kupatikana Taratibu ngumu za usajili au vibali kutozingatia viwango vya ubora au usalama

6. Hatari za Miundombinu kukatika kwa umeme au maji mara kwa mara Barabara mbovu zinazochelewesha usafirishaji gharama kubwa za usafirishaji huduma duni za mawasiliano na mtandao Uharibifu wa vifaa au mashine kutokana na mazingira
7. Hatari za Rasilimali Watu Wafanyakazi kukosa ujuzi na mafunzo ya mara kwa mara Uzalendo mdogo au kutoridhika kwa wafanyakazi Migogoro baina ya wafanyakazi au na waajiri Kutokuwepo kwa sera bora za ajira kutokuwa na motisha au mfumo wa kuhamasisha
wafanyakazi.

8. Hatari za Ufuatiliaji na Taarifa kukosa takwimu sahihi za mauzo au uzalishaji kukosekana kwa taarifa sahihi za masoko na wateja kushindwa kugundua mapema changamoto zinazokuja kukosa mfumo wa kuripoti na kufuatilia maendeleo kutojua mahitaji halisi ya soko kwa wakati

9. Hatari za Washirika na Watoa Huduma
Washirika kushindwa kutimiza ahadi walizoweka.Mikataba mibovu isiyo na ulinzi wa kutosha.kukosekana kwa maelewano ya kibiashara.Kutegemea mshirika mmoja kwa huduma muhimu.
Kucheleweshwa kwa bidhaa au huduma.

10. Hatari za Kisaikolojia na Maamuzi Mabaya Maamuzi ya haraka bila uchambuzi wa kina.Kuongozwa na hofu au shinikizo la soko. Kukosa mwelekeo wa muda mrefu (long-term vision).Kukosa msaada wa kitaalamu au ushauri wa biashara. Kutokuwa tayari kwa mabadiliko au majanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *