Posted in

187+ Nafasi za Ajira Serikalini, Nafasi za Kazi UTUMISHI


Fursa za kazi serikalini | Nafasi za ajira serikalini

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni chombo cha serikali chenye hadhi ya Idara huru kilichoanzishwa mahsusi kuwezesha mchakato wa uajiri wa watumishi katika Utumishi wa Umma. Chombo hiki kilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho kwa Sheria Na. 18 ya mwaka 2007, kifungu cha 29(1).

Dira yetu:


Kuwa Kituo Bora cha Umahiri katika Utumishi wa Umma katika ukanda huu.

Dhamira yetu:


Kutekeleza shughuli za uajiri wa watumishi wa umma kwa kutumia mbinu za kisasa kwa kuzingatia misingi ya usawa, uwazi na sifa pamoja na kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala yanayohusiana na ajira. Rasilimali watu ni nguzo muhimu katika utoaji wa huduma za umma, hivyo PSRS imepewa jukumu la kuajiri watumishi wa umma kwa njia ya haki, uwazi na kwa wakati; huku ikizingatia na kuhakikisha ubora na upatikanaji kwa waombaji wote ili kutoa huduma sawa kwa Watanzania wote.

Lengo letu ni kuboresha huduma za ajira serikalini kwa kuzingatia taratibu na kanuni zetu, na wakati huo huo kuimarisha uhusiano mzuri na wadau wetu. Chombo hiki ni mwajiri wa fursa sawa kwa wote.

Chombo hiki kinakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania kujaza nafasi mpya za kazi.


BONYEZA HAPA KUONA NAFASI ZA KAZI SERIKALINI ZILIZOPO MWEZI HUU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *